Wednesday, 3 December 2014

KARIBU MSIMBAZI DAN SSERUNKUMA



Jembe jipya la Simba Dan Sserunkuma anatarajiwa kutua nchini leo kumalizana na Simba. Mganda huyo anatarajiwa kuchukua nafasi ya Mkenya Paul Kiongera ambaye ameondolewa kwenye orodha ya wachezaji wa Simba SC msimu huu kutokana na majeraha.

Thursday, 5 June 2014

MAXIMO NA YANGA KUNA JIPYA?

Timu ya YANGA inaonesha nia ya dhati ya kumleta kundini  kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbrazili Marcio Maximo. Kocha huyo ambae anasifa ya kandanda safi ya pasi fupi fupi anakaribia kabisa kujiunga na Yanga kwa msimu ujao wa ligi endapo watakubaliana na masharti yake.

RICKIE LAMBERT AINGIA KITANZI NA LIVERPOOL

Rickie Lambert alikamilisha deal ya kuichezea Liverpool wiki iliyopita akiwa mchezaji wa kwanza kujiunga na kikosi hicho cha majogoo wa Anfield kwa Kitita cha paundi milioni 4. 
Akiwa na umri wa miaka 32 Rickie aliyezaliwa  katika jiji la Liverpool na aliyekwenye kikosi cha Uingereza kilichoko njiani kwenda Brazili, anahamia Liverpool akitokea Southampton ambako alikuwa na msimu mzuri huku akicheza mechi 39  na kufunga jumla ya magoli 14 hali akitoa ushirikiano wa magoli 10

DIEGO COSTA KUMALIZANA NA CHELSEA

Mshambuliaji anayeibukia wa Atletico Madrid, Diego Costa amekamilisha vipimo vya afya yake na Chelsea katika uhamisho unaotegemewa kufikia kisasi cha paundi milioni 32. 
Mzaliwa huyo wa Brazili katika jimbo la Lagarto mwenye umri wa miaka  25, ambaye ni sehemu ya timu ya taifa ya Uispania anatakiwa na kocha mkorofi wa maneno Jose  Mourinho ili kuwezesha kikosi cha Chelsea kutwaa mataji msimu ujao. 

Monday, 2 June 2014

TAIFA STARS YAIPA KIBANO ZIMBABWE

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka kidedea baada ya kutoka sare na timu ya taifa ya Zimbabwe (The Worriors ) kwenye mchezo uliochezwa Jana mjini Harare. Kwenye mchezo huo sare ya 2 - 2 ilishuhudiwa na mashabiki wapatao 50 000 waliofika  kushuhudia. 

MOYES "NLIKUWA NA MIPANGO YA MUDA MREFU"

Kocha aliyetupiwa virago wa Manchester United David Moyes amesema hana mpango wowote na Kilabu hiyo kwa sasa wala kwa wakati ujao, japo amesema alikuwa na mipango ya muda mrefu ya timu lakini hakupewa

QATAR KUONDOLEWA HAKI YA KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2022

Kutokana na kashfa inayokabili mchakato mzima wa kuiteua Qatar kuwa mwandaaji wa kombe la dunia 2022, huenda haki hiyo ikaondolewa endapo itathibitika kuwa maofisa wa ngazi za juu za vyama mbalimbali vya soka walipewa mlungula kupitisha nchi hiyo.

Thursday, 29 May 2014

MMILIKI WA MANCHESTER UNITED AAGA DUNIA


Aliyekuwa mmliki wa Timu ya Manchester United Malcolm Glaze amefariki dunia jana asubuhi akiwa na umri wa miaka 86. Glaze aliinunua Man U mwaka 2005 na kupata upinzani mkubwa wa mashabiki, wakiwa wanaona kuwa anaitumia Klabu hiyo kama njia ya kulipa madeni yake. 

Monday, 26 May 2014

LAMPARD NA REO FERDINAND KUJIUNGA NA QPR

Kocha wa QPR Harry Redknapp anajipanga kuwarudisha kundini wachezaji  wawili, Mlinzi wa kati wa Manchester Unite Reo Ferdinand (35) and Kiungo wa Chelsea aliyemaliza mkataba wake Frank Lampard (35) 
Timu ya QPR imefuzu kucheza premier baada ya kuwafunga Derby kwa goli moja la dakika za mwisho. Kocha huyo anatamani kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji watakaohimili mikiki ya ligi hiyo yenye mvuto duniani.

Saturday, 24 May 2014

DEAL IMEKAMILIKA DAVID LUIZ KWENDA UFARANSA

Habari kutoka mtandao wa Chelsea unasema kuwa umekubaliana na timu ya Paris Saint-Germain kumuuza mchezaji wao wa nafasi ya ulinzi, machachari David Luiz kwa dau kubwa kuwahi kutokea kwa mlinzi. 

Tuesday, 20 May 2014

HACHIM MASTOUR NI NOMAAAAA

Timu ya AC Millan imeamua kumpandisha kinda wao Hachim Mastour kwenye kikosi chao cha kwanza. Mtoto huyo mwenye asili ya Moroko aliamia Ac Millan akitokea Reggiana kwa uamisho wa Euro laki tano mwaka 2012 na amekuwa akijumuishwa kwenye kikosi cha vijana cha Italy

WENGER KUSAINI MKATABA MPYA

 
Arsenal inajiandaa kumpa mkataba wenye thamani ya paundi milioni 24 Mfaransa mbahili Arsen Wenger muda mfupi ujao. Inasemekana pia kuwa, mzee huyo atapewa kitita cha paundi milioni 100 kukiimarisha kikosi chake chenye safu mbovu ya ushambuliaji. 

LUIS ENRIQUE KOCHA MPYA BARCELONA

Baada ya kumaliza msimu wa 2013-14 bila taji lolote, kocha Martino aliamua kumwaga manyanga, na kutoa fursa kwa Barcelona kumtangaza kiungo wake wa zamani Luis Enrique kuchukua mikoba hiyo.

LOUIS VAN GAAL KOCHA MPYA MAN UNITED

Manchester United wamempa shavu Mholanzi Louis Van Gaal kuwa mwalimu wa kikosi hicho mara baada ya kumali zika kwa fainali za kombe la dunia mwaka huu.

Monday, 19 May 2014

TAIFA STARS WAPATA USHINDI MWEMBAMBA


Timu ya Taifa stars ya Tanzania imepata ushindi mwembamba dhidi ya Zimbabwe kwenye mchezo ulopigwa kunako uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania. 

JUVENTUS BINGWA MPYA SERIE A 2013-14

Timu ya Bibi kizee cha Turin, Juventus wameibuka mabingwa wapya wa Serie A kwa kuichapa Cagliari kwa magoli matatu bila majibu na kufikisha pointi 102 ikiwa na ubigwa wao wa mara ya tatu mfulululizo na kuweka rekodi ya kumaliza michezo 38 ikiwa na magoli 101. 

Sunday, 18 May 2014

ARSENAL MBABE KOMBE LA FA 2013/14

Lilikua goli la Aaron Ramsey dakika ya 109 lililoipa Arsenal Ndoo ya FA mbele ya Hull City kunako dimba la Wembley jana Usiku na kuondoa ukame wa vikombe kwa Arsenal kwa miaka 8 miezi 11 na siku 26.

Friday, 16 May 2014

YASEMAVYO MAGAZETI YA UINGEREZA MEI 16

DELE ALLI
Chelsea, Liverpool na Arsenal wanamnyatia kiungo kinda miaka 18 wa MK Dons anayelinganishwa na Steven Gerald kwa namna ya uchezaji wake (Daily express)

MANCHESTER CITY MBIONI KUMNASA BEKI WA ROMA


Timu ya Manchester city ipo kwenye nafasi nzuri kumnasa beki mwenye mapafu ya mbwa kutoka Morocco Mehdi Benatia anayekipiga kunako Ac Roma ya Italia


ARSENAL KUMSAJILI SOLOMON KALOU

Umbea toka kwenye magazeti ya udaku nchini Uingereza yanamhusisha Solomon Kalou anayekipiga kwenye ligi ya Ufaransa na Arsenal 

Thursday, 15 May 2014

SEVILLA BINGWA MPYA KOMBE LA EUROPA 2013/14



Mkosi wa kutokutwaa kombe la Ueropa umeendelea kuiandama timu ya Benefica ya Ureno baada ya jana usiku kukabithiwa kichapo cha matuta manne kwa mawili kutoka kwa vijana wa Uhispania Sevilla.

Wednesday, 14 May 2014

HIKI NDIO KIKOSI CHA GHANA KUELEKEA BRAZILI 2014

 Ghana wanaelekea nchini Brazili wakiwa na kikosi kilichosheheni wachezaji wenye uzoefu mkubwa. Wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza uwakilishi muhimu kwenye robo fainali huko bondeni kwa hayati Madiba miaka minne iliyo pita, wanakibarua kikubwa kupambana na wenzio kwenye kundi lao la kifo (G) Linalojumuisha wababe kama, USA, Wareno na Wajerumani.

HAWA NDIO IVORY COAST .....2014

 Kocha wa Ivory Coast, Sabri Lamouchi ametangaza wasakata kabumbu watakao iwakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya Dunia mwanzoni mwa mwezi wa sita nchini Brazili.

KIKOSI CHA HISPANIA SAFARINI KWENDA BRAZILI 2014



WAHISPANIA wamekuwa wazuri kwa miaka ya hivi karibuni kwenye soka la kitaifa na kimataifa.Walishinda kombe la dunia kwa mara ya kwanza miaka minne iliyopita, kama hiyo haitoshi waka twaa ndoo ya Ulaya mwaka 2008 na mwaka 2012. 
Watapenda kuendelea na mdundo huo, ama kuuongezea kasi kidogo mwezi ujao nchini Brazili.

JE WAKIJUA KIKOSI CHA BRAZIL.....2014?

 Mwanzoni mwa mwezi huu wa tano, kocha mkuu wa timu ya Brazili mtaalamu Luiz Felipe Scolari ametangaza vijana wake watakao iwakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya kombe la dunia itakayoanza kusakatwa kwenye miji kazaa nchini humo. 
vijana hao ni kama ifuatavyo. 
Magolikipa: