Monday, 2 June 2014

MOYES "NLIKUWA NA MIPANGO YA MUDA MREFU"

Kocha aliyetupiwa virago wa Manchester United David Moyes amesema hana mpango wowote na Kilabu hiyo kwa sasa wala kwa wakati ujao, japo amesema alikuwa na mipango ya muda mrefu ya timu lakini hakupewa
fursa ya kuitekeleza. Hata hivyo amekiri kuwa na support kubwa kutoka kwa kocha mstaafu Alex Ferguson, na anakiri kuwa  kwa sasa ameshasonga mbele na hatazami nyuma tena. 
David moyes alitupiwa virago rasmi mnamo mwezi wa nne baada ya kuwa mwalimu wa timu hiyo kwa miezi kumi (10) tu na kupelekea Manchester kuwa kwenye nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza.
Hata hivyo Moyes anakiri kuwa na offers mbili mpaka sasa na anafikiria aichukue gani kati ya hizo.

No comments: