Mshambuliaji anayeibukia wa Atletico Madrid, Diego Costa amekamilisha vipimo vya afya yake na Chelsea katika uhamisho unaotegemewa kufikia kisasi cha paundi milioni 32. Mzaliwa huyo wa Brazili katika jimbo la Lagarto mwenye umri wa miaka 25, ambaye ni sehemu ya timu ya taifa ya Uispania anatakiwa na kocha mkorofi wa maneno Jose Mourinho ili kuwezesha kikosi cha Chelsea kutwaa mataji msimu ujao.
Diego costa ameifungia timu yake ya Atletico Madrid jumla ya magoli 52 kwa msimu uliopita anahamia Chelsea kuondoa shida ya mfungaji anayoilalamikia kocha wa timu hiyo mtata Jose Mourinho.
Kwa uhamisho huo ni dhahiri kuwa Chelsea hawaitaji tena wawili kati ya washambuliaji wake waliopo, hali kiungo Frank lampard akiwa njiani kuondoka, na uhamisho wa David Luiz ukiwa umekamilika.
No comments:
Post a Comment