Monday, 2 June 2014

TAIFA STARS YAIPA KIBANO ZIMBABWE

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka kidedea baada ya kutoka sare na timu ya taifa ya Zimbabwe (The Worriors ) kwenye mchezo uliochezwa Jana mjini Harare. Kwenye mchezo huo sare ya 2 - 2 ilishuhudiwa na mashabiki wapatao 50 000 waliofika  kushuhudia. 

Ilikuwa dakika ya 13 pale ambapo Danny Phiri alipowainua mashabiki wa Zimbabwe na kufanya matokeo kuwa 1 - 1, kutokana na Goli moja waliopigwa vijana hao wa Mzee Mugabe jijini Dar es salaam wiki mbili zilizopita.
Kunako dakika ya 26  Nadir Haroub aliamsha matumaini kwa Taifa stars baada ya kuukwamisha mpira wa kona na kufanya matokeo kuwa magumu kwa Zimbabwe. Dakika ya 46 Thomas ulimwengu alitumia vyema udhaifu wa  beki Erick Chipeta na kufanya vijana wa Kikwete kuwa na matumaini makubwa ya kufuzu, hata hivyo goli hilo lilidumu kwa muda wa dakika 9 tu baada ya kiungo wa Zimbabwe Willard Katsande kusawazisha dakika 55 na kufanya matokeo kuwa 2- 2. 
Hadi dakika ya mwisho ya mchezo, Tanzania 2 na Zimbabwe 2.  Kwa matokeo hayo, Timu ya Tanzania imepita hatua hiyo na sasa kusubiri kupambana na timu ya Msumbiji

No comments: