Sunday, 5 July 2015

CHILE WASHINDA COMBE LA COPA AMERIKA

Waandaji wa kombe la copa america Chile, jana wameibuka wababe  wa kombe hilo baada ya kuwashinda wapinzani wao wa zamani Argentina kwa matuta kwenye uwanja wa  Estadio Nacional mjini Santiago, baada ya mtanange huo kuisha kwa draw ya mayai hata baada ya dakika 120 .

Chile wameshinda kikombe hicho kwa mara ya kwanza kwenye historia yao ya soka mbele ya mashabiki wenye mshawasha wakikombe hicho. hahasa baada ya kukisubiri. Chile wameonesha uwezo mzuri wa kusakata kabumbu haswa baada ya timu kama za Brazili, Argentina na Uruguay kuonesha viwango vya chini.

Wednesday, 3 December 2014

KARIBU MSIMBAZI DAN SSERUNKUMA



Jembe jipya la Simba Dan Sserunkuma anatarajiwa kutua nchini leo kumalizana na Simba. Mganda huyo anatarajiwa kuchukua nafasi ya Mkenya Paul Kiongera ambaye ameondolewa kwenye orodha ya wachezaji wa Simba SC msimu huu kutokana na majeraha.

Thursday, 5 June 2014

MAXIMO NA YANGA KUNA JIPYA?

Timu ya YANGA inaonesha nia ya dhati ya kumleta kundini  kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbrazili Marcio Maximo. Kocha huyo ambae anasifa ya kandanda safi ya pasi fupi fupi anakaribia kabisa kujiunga na Yanga kwa msimu ujao wa ligi endapo watakubaliana na masharti yake.

RICKIE LAMBERT AINGIA KITANZI NA LIVERPOOL

Rickie Lambert alikamilisha deal ya kuichezea Liverpool wiki iliyopita akiwa mchezaji wa kwanza kujiunga na kikosi hicho cha majogoo wa Anfield kwa Kitita cha paundi milioni 4. 
Akiwa na umri wa miaka 32 Rickie aliyezaliwa  katika jiji la Liverpool na aliyekwenye kikosi cha Uingereza kilichoko njiani kwenda Brazili, anahamia Liverpool akitokea Southampton ambako alikuwa na msimu mzuri huku akicheza mechi 39  na kufunga jumla ya magoli 14 hali akitoa ushirikiano wa magoli 10

DIEGO COSTA KUMALIZANA NA CHELSEA

Mshambuliaji anayeibukia wa Atletico Madrid, Diego Costa amekamilisha vipimo vya afya yake na Chelsea katika uhamisho unaotegemewa kufikia kisasi cha paundi milioni 32. 
Mzaliwa huyo wa Brazili katika jimbo la Lagarto mwenye umri wa miaka  25, ambaye ni sehemu ya timu ya taifa ya Uispania anatakiwa na kocha mkorofi wa maneno Jose  Mourinho ili kuwezesha kikosi cha Chelsea kutwaa mataji msimu ujao. 

Monday, 2 June 2014

TAIFA STARS YAIPA KIBANO ZIMBABWE

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka kidedea baada ya kutoka sare na timu ya taifa ya Zimbabwe (The Worriors ) kwenye mchezo uliochezwa Jana mjini Harare. Kwenye mchezo huo sare ya 2 - 2 ilishuhudiwa na mashabiki wapatao 50 000 waliofika  kushuhudia. 

MOYES "NLIKUWA NA MIPANGO YA MUDA MREFU"

Kocha aliyetupiwa virago wa Manchester United David Moyes amesema hana mpango wowote na Kilabu hiyo kwa sasa wala kwa wakati ujao, japo amesema alikuwa na mipango ya muda mrefu ya timu lakini hakupewa

QATAR KUONDOLEWA HAKI YA KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2022

Kutokana na kashfa inayokabili mchakato mzima wa kuiteua Qatar kuwa mwandaaji wa kombe la dunia 2022, huenda haki hiyo ikaondolewa endapo itathibitika kuwa maofisa wa ngazi za juu za vyama mbalimbali vya soka walipewa mlungula kupitisha nchi hiyo.

Thursday, 29 May 2014

MMILIKI WA MANCHESTER UNITED AAGA DUNIA


Aliyekuwa mmliki wa Timu ya Manchester United Malcolm Glaze amefariki dunia jana asubuhi akiwa na umri wa miaka 86. Glaze aliinunua Man U mwaka 2005 na kupata upinzani mkubwa wa mashabiki, wakiwa wanaona kuwa anaitumia Klabu hiyo kama njia ya kulipa madeni yake. 

Monday, 26 May 2014

LAMPARD NA REO FERDINAND KUJIUNGA NA QPR

Kocha wa QPR Harry Redknapp anajipanga kuwarudisha kundini wachezaji  wawili, Mlinzi wa kati wa Manchester Unite Reo Ferdinand (35) and Kiungo wa Chelsea aliyemaliza mkataba wake Frank Lampard (35) 
Timu ya QPR imefuzu kucheza premier baada ya kuwafunga Derby kwa goli moja la dakika za mwisho. Kocha huyo anatamani kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji watakaohimili mikiki ya ligi hiyo yenye mvuto duniani.