Aliyekuwa mmliki wa Timu ya Manchester United Malcolm Glaze amefariki dunia jana asubuhi akiwa na umri wa miaka 86. Glaze aliinunua Man U mwaka 2005 na kupata upinzani mkubwa wa mashabiki, wakiwa wanaona kuwa anaitumia Klabu hiyo kama njia ya kulipa madeni yake. Hata hivyo chini ya umiliki wake, amewezesha timu hiyo kutwaa makombe matano ya premia na kombe moja la klabu bingwa ya Ulaya alimaarufu kama UEFA mwaka 2008
Glaze alikuwa pia mmiliki wa timu ya mpira wa miguu wa marekani ijulikanayo kama NFL ya TAMPA BAY BUCCANEERS, aliwaachia wanawe wawili Avram and Joel mwaka 2006 kuendesha shughuli za klub wakati alipopata ugonjwa wa kiharusi.
Poleni sana mashabiki wa Man united
No comments:
Post a Comment