Monday, 19 May 2014

TAIFA STARS WAPATA USHINDI MWEMBAMBA


Timu ya Taifa stars ya Tanzania imepata ushindi mwembamba dhidi ya Zimbabwe kwenye mchezo ulopigwa kunako uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania. 

Goli hilo lililowekwa kimiani na mshambuliaji John Bocco kwenye dakika ya 13 baaada ya kuunganisha pasi murua ya Thomas Ulimwengu, lilidumu hadi kipenga cha mwisho kinalia.
Stars itahitaji kujipanga vema kama kweli wanahitaji kuwepo kwenye nafasi nzuri ya kushiriki Kombe la Mataifa ya Africa mwaka ujao 2015. 
Hata hivyo kuna haja ya kocha mpya kuachana na utamaduni wa kujaza kikosi hicho sura zile zile na badala yake kujenga timu ya kiushindani zaidi.

No comments: