Mkosi wa kutokutwaa kombe la Ueropa umeendelea kuiandama
timu ya Benefica ya Ureno baada ya jana usiku kukabithiwa kichapo cha matuta
manne kwa mawili kutoka kwa vijana wa Uhispania Sevilla.
Kwa matokeo hayo ya kusikitisha kwa benefica ambao
walipoteza msimu uliopita kwa Chelsea kwa kichapo cha magoli mawili kwa moja….jana
walikuwa na hamu ya kunyanyua ndoo hiyo bila mafanikio.
Alikuwa golikipa wa benefica Beto aliyekuwa na kisimati,
baada ya kuchomoa penalti mbili toka kwa
mshambuliaji wa Benefica Oscar Cardozo na Rodrigo aliyepiga penalti fyongo, na
kuwafanya Sevilla kuibuka na ushindi wa Penalti 4 kwa 2 za Benefica.
Ilikuwa penalti ya Kevin Gameiro iliyosababisha mashabiki
wa Sevilla kunyanyuka na kupiga mayowe ya shangwe na kuwafanya Benefica wasio na
bahati tangu walipotwaa kombe hilo kwa mara ya pili mwaka 1962
Kwa matokeo hayo, ni wazi kuwa Uhispania imeimarika
kisoka, hali tukisubiri kuona wababe wa La Liga Atletico Madrid wakikichapa na
Real Madrid tarehe 24 mei kunako dimba la Estadio da Luz

No comments:
Post a Comment