Ghana wanaelekea nchini Brazili wakiwa na kikosi kilichosheheni
wachezaji wenye uzoefu mkubwa. Wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza uwakilishi
muhimu kwenye robo fainali huko bondeni kwa hayati Madiba miaka minne iliyo
pita, wanakibarua kikubwa kupambana na wenzio kwenye kundi lao la kifo (G)
Linalojumuisha wababe kama, USA, Wareno na Wajerumani.Hata hivyo Bl
ack stars wanajisifia watu kama, Prince Boateng na mkongwe Michael Essien pamoja na Asamoah Gyan alietumwa hela kwa Waarabu.
Kocha wao mzawa James Kwesi Appiah aliechukua mikoba hiyo mwaka
2012 na kuwa kocha wa kwanza kabisa wa Kiafrica kuchukua majukumu ya kufunza
Ghana kwenye michuano ya kombe la dunia anategemewa kufanya vyema zaidi,
haswa kwa kuwa na kikosi hicho kwa muda wa kutosha sasa.
Kikosi hicho ni kama ifutatavyo
Magolikipa ni:
Fatau Dauda (Orlando Pirates),
Adam
Kwarasey (Stromsgodset),
Stephen Adams (Aduana Stars).
Walinzi: Samuel
Inkoom (Platanias),
Daniel Opare (Standard Liege),
Harrison Afful (Esperance),
Jeffrey Schlupp (Leicester),
John Boye (Rennes),
Jonathan Mensah (Evian), Jerry
Akaminko (Kisehirspor), Rashid Sumalia (Mamelodi Sundowns).
Viungo: Michael
Essien (AC Milan), Sulley Muntari (AC Milan), Rabiu Mohammed (Kuban Krasnodar),
Kwadwo Asamoah (Juventus), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese), Afriyie Acquah
(Parma), Christian Atsu (Vitesse), Albert Adomah (Middlesbrough), Andre Ayew
(Marseille), Mubarak Wakaso (Rubin Kazan).
Washambuliaji: Asamoah
Gyan (Al Ain), Kevin-Prince Boateng (Schalke 04), Abdul Majeed Waris
(Valenciennes), Jordan Ayew (Sochaux), David Accam (Helsingborg).
No comments:
Post a Comment