Sunday, 18 May 2014

ARSENAL MBABE KOMBE LA FA 2013/14

Lilikua goli la Aaron Ramsey dakika ya 109 lililoipa Arsenal Ndoo ya FA mbele ya Hull City kunako dimba la Wembley jana Usiku na kuondoa ukame wa vikombe kwa Arsenal kwa miaka 8 miezi 11 na siku 26.

Wakiwa wapo nyuma kwa magoli mawili yaliowekwa kimiani na Chester dakika ya 4 na lile la Davies dakika ya 8, Arsenal walijitutumua na kurudisha magoli hayo kupitia Cazola dakika ya 17 na kuwarudisha uwanjani Arsenal wakiwa na mshambuliaji wao mlamba midomo Giroud ambaye hakuwa na msaada kwa timu hiyo hapo Jana.
Kipindi cha pili kilianza Arsenal wakiwa nyuma kwa magoli mawili kwa moja, na kuonesha mchezo usioridhisha haswa kwa Mjerumani Podoski na Mfaransa Giroud ambao hawakucheza kiushindani kwenye mchezo huo. Hata hivyo kuingizwa kwa Sanongo kulirudisha matumaini na kuamsha hari ya ushindani. 
Dakika ya 71, Koscielny aliwaamsha mashabiki wa arsenal waliokuwa na mshawasha wa kushinda kikombe baada ya kuwa na simanzi kwa muda mrefu sasa. 
Hadi kipenga cha mwisho kinalia, Arsenal 3 Hully City 2.Matokeo ambayo yanaipa Arsenal Ubingwa wa FA na kuondoa gundu ya muda mrefu. 
Hongereni Arsenal

No comments: