Tuesday, 20 May 2014

WENGER KUSAINI MKATABA MPYA

 
Arsenal inajiandaa kumpa mkataba wenye thamani ya paundi milioni 24 Mfaransa mbahili Arsen Wenger muda mfupi ujao. Inasemekana pia kuwa, mzee huyo atapewa kitita cha paundi milioni 100 kukiimarisha kikosi chake chenye safu mbovu ya ushambuliaji. 
   Mzee huyo anayesifika kwa ubahili amepewa shavu hilo baada ya kumaliza miaka kama tisa hivi ya ukame wa vikombe klabuni hapo na kuonesha mwanga kwamba bado anaweza kuleta vikombe msimu ujao.
  Hata hivo magazeti ya nchini Uingereza yanadakua kuwa anamshawasha wa kuwasajili Karim Benzema wa Real na Mario Mandzukic wa Buyern japo atapata upinzani kutoka kwa Chelsea.

No comments: