Waandaji wa kombe la copa america Chile, jana wameibuka wababe wa kombe hilo baada ya kuwashinda wapinzani wao wa zamani Argentina kwa matuta kwenye uwanja wa Estadio Nacional mjini Santiago, baada ya mtanange huo kuisha kwa draw ya mayai hata baada ya dakika 120 .
Chile wameshinda kikombe hicho kwa mara ya kwanza kwenye historia yao ya soka mbele ya mashabiki wenye mshawasha wakikombe hicho. hahasa baada ya kukisubiri. Chile wameonesha uwezo mzuri wa kusakata kabumbu haswa baada ya timu kama za Brazili, Argentina na Uruguay kuonesha viwango vya chini.
Kwa upande wa Argentina chini ya mchezaji mahiri wa Dunia Lionel Messi, walionekana wazi wakicheza kupata draw ili kujaribu bahati yao kwenye matuta, lakini hali haikuishia hivyo baada ya kujikuta wanatolewa kwa matuta manne (4) kwa moja (1)
Hata hivyo kocha wa Argentina Tata Martino alifanya mabadiliko ya kushangaza wengi na kuliacha jembe la Juventus Carlos Tevez likiwa limekalia mbao.
Walikuwa chile waliotawala mchezo huo kwa asilimia 57% huku Argentina wakiwa na asilimia 43% tu.
Matuta mawili ya argentina yaliopigwa na Éver Banega na Gonzalo Higuaín ndio yalihitimisha mtanange huo na kuwapa Chile ubingwa. Matuta ya Chile yaliwekwa kimiani na Matías Fernández, Arturo Vidal, Charles Aránguiz na Alexis Sánchez

No comments:
Post a Comment