Wednesday, 3 December 2014

KARIBU MSIMBAZI DAN SSERUNKUMA



Jembe jipya la Simba Dan Sserunkuma anatarajiwa kutua nchini leo kumalizana na Simba. Mganda huyo anatarajiwa kuchukua nafasi ya Mkenya Paul Kiongera ambaye ameondolewa kwenye orodha ya wachezaji wa Simba SC msimu huu kutokana na majeraha.

Mshambuliaji huyo alikuwa akikipiga kunako klabu ya Gor Mahia ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL) na sasa anakaribia kuhamishia makali yake kunako mitaa yenye pilika pilika nyingi ya Msimbazi Jijiini Dar es salaam. Hata hivo Gor wameelezea masikitiko yao kupitia katibu wao mkuu Chris Omondi ya kumkosa mfumania nyavu huyo mahiri kwa msimu wao huu baada ya Jembe hilo kugoma kusaini mkataba mpya na wakongwe hao wa KPL na badala yake kufuata mkataba mnono Msimbazi.
Simba wapo katika mchakato wa kuimarisha kikosi chao baada ya kufanya ndivyo sivyo kwenye mechi zake za mzunguko wa kwanza wa Ligi. Mbali na mshambuliaji huyo, Simba wamejitaba kuimarisha kikosi hicho na kuwa moto kwa mzunguko ujao wa ligi. 

No comments: