Thursday, 5 June 2014

MAXIMO NA YANGA KUNA JIPYA?

Timu ya YANGA inaonesha nia ya dhati ya kumleta kundini  kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbrazili Marcio Maximo. Kocha huyo ambae anasifa ya kandanda safi ya pasi fupi fupi anakaribia kabisa kujiunga na Yanga kwa msimu ujao wa ligi endapo watakubaliana na masharti yake.


Mbrazil Marcio Maximo,anawataka Yanga kwanza wakubaliane na haja yake ya kuja na mtaalamu wa viungo Itamar Amorim ili kumsaidia, lakini wakalia Viti wa Yanga hawajakubaliana na hilo haswa ukizingatia kuwa mtaalamu huyo atataka dola 4000 kama mshahara kwa mwezi hali Yanga wanataka kocha huyo afanye kazi na mzawa Boniface Mkwasa. 
Lakini pia, kocha huyo anahitaji mshahara wa dola 15,000 kwa mwezi sawa na milioni 25 za Kitanzania, ambazo Yanga wanabembelezea zipungue kidogo.Madai mengine ya nyumba yenye hadhi kama aliyokuwa akikaa wakati akiwa nchini ni moja wapo ya madai ya kocha huyo. Lakini Maximo pia ametaka apewe usafiri mzuri wa kisasa atakaoutumia katika kazi zake, hata hivyo Yanga wamemwambia watampa Prado la kisasa.
Mshawasha wangu ni kuwa, kama makocha wa kizawa wakipewa mishahara mizuri na marupurupu nusu ya wageni, wanaweza wakaleta mabadiliko kwenye soka la bongo. Muhimu ni kuwapa majukumu na kuwataka kuyatimiza bila viongozi kuwachagulia nani asajiliwe na nani asisajiliwe. 

No comments: